Jumatatu, 29 Januari 2018

Kisa cha Rais Trump kujibizana na mwanamuziki Jay-Z


Rais wa Marekani Donald Trump amemjibu Jay-Z baada ya mwanamuziki huyo wa muziki wa Rap kumuita "mdudu hatari'' na kumkaripia kwa namna anavyowachukulia watu weusi.
Donald Trump and Jay-Z 

Katika ujumbe kwenye Twitter Bw Trump alisema kuwa "kiwango cha Wamarekani wasio na ajira kimeripotiwa kuwa cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa!" kwa sababu ya sera zake.

WaMarekani wenye asili ya Afrika wasio na ajira niasilimia 6.8%, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi zaidi kurekodiwa.

Lakini wakosoaji wanasema kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilianza kuimarika wakati wa rais Obama na kwamba ukosefu wa ajira miongoni mwa watu weusi umesalia kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwao kuliko miongoni mwa wazungu.

Alipokuwa katika kipindi cha televisheni ya CNN cha Van Jones Show, Jay-Z alisema kuwa kuangazia viwango vya ukosefu wa ajira ni " kukosa ufahamu wa mambo".
"Sio suala la ukosefu wa pesa pekee lenye umuhimu … pesa hazileti furaha... hazileti.

Hii ni kushindwa kuelewa ukweli. Uwachukulie watu kama binadamu ...hilo ndio suala kuu la muhimu."Aidha amesema kuwa kuchaguliwa kwa Bw Trump kulitokana na kushindwa kutatuliwa kikamilifu kwa masuala kadhaa.

"Umepuliza manukato katika debe la taka," alisema. "Unapofanya hivyo ni kwamba unawafanya wadudu hatari kufika. Unapopuliza kitu basi unasababisha kuzaliwa kwa wadudu hatari kwa sababu haungazii tatizo halisi."

"Hauchukui taka nje, unaendelea kupuliza dawa juu yake ili kulifanya debe la taka kukubalika. Vitu hivyo vinapokuwa, huwa unabuni mdudu hatari . Na kwa sasa mdudu hatari tuliyr naye ni Donald Trump, mdudu hatari."

Jay-Z alimuunga mkono Barack Obama wakati wauongozi wake, na alimsifia Bi Hillary Clinton katikauchaguzi wa mwaka 2016 ambapo Bwana Trump alishinda

Pia aliulizwa kuhusu madai ya rais Trump kuyataja mataifa ya Afrika kuwa "machafu" au mataifa ya "mabwege".
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.

Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.
Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani."Inasikitisha na inaumiza," alisema Jay-Z.

 "Kila mtu anahisi hasira. Baada ya hasira, inasikitisha sana kwa sababu ni kama ana dharau kwa watu wote .
"Rais Trump amekanusha madai yote kwamba ya ubaguzi dhidi yake.Alisema kuwa lugha aliyoitumia ilikuwa ni ya ''ukali '' lakini anakana kutumia neno linaloripotiwa.

Ijumaa, 19 Januari 2018

Mwanamke aliyechagua ng'ombe badala ya ndoa India

Selvarani Kanagarasu, mfanyikazi anayetegemea mshahara wa siku kutoka jimbo la kusini nchini India la Tamil Nadu amekataa kuolewa na badala yake akaamua kumiliki ng'ombe wa mchezo wa kupigana kwamafahali kulingana na mwandishi wa BBC Tamil Pramilan Krishna.
Selvarani Kanagarasu
 aliyekataa kuolewa ili kumfuga ngombe huyo

Bi Kanagarasu mwenye umri wa miaka 48 alikuwa kijana wakati alipoamua kwamba alitaka kufuata nyayo za babake na babu yake ambao walifuga ng'ombe wa kiume walioshindana katika mchezo ya jimbo hilo ya kupigana kwa mafahali kwa jina Jallikatu.
Jallikatu ni mchezo maarufu kwa karne kadhaa jimboni Tamil Nadu na huchezwa wakati wa msimu wa kuvuna wa Pongal mwezi Januari.
Maelfu ya watu hufukuza ng'ombe ili kuchukua zawadi zilizowekwa katika pembe zao.
Mchezo huo haukichezwa kwa kipindi cha miaka miwili kufuatia marufuku ya mahakama ya juu kwa madai kwamba walikuwa wakiwafanyia wanyama hao ukatili.
Lakini kufuatia maandamano katika jimbo hilo, serikali ya jimbo hilo iliamua kuruhusu kuendeleaa mnamo mwezi Januari 2017 na hivyobasi kupuuzilia mbali marufuku iliowekwa.
''Babangu na babu yangu walifuga ngombe na kuwachukulia kama watoto wao'', alisema
Jukumu la kuendeleza utamaduni wa kifamilia lingemwangukia nduguze bi Kanagarasu, lakini anasema hawakuwa na muda wa kuwaangalia wanyama hao.
Hivyobasi akaamua kuchukua jukumu hilo.
Ng'ombe anayemfuga ,kwa jina Ramu ni mnyama mwenye umri wa miaka 18 ambaye ni lejendari katika eneo hilo.
Shindano la Jalikattu katika jimbo la Tamil Nadu India

Ramu ameshinda mashindano matano kati ya saba ya Jallikattu ambayo alishiriki, akishinda zawadi kama vile sare na sarafu ya dhahabu kwa mmiliki wake.
''Ramu ni mwanangu wa kiume .Alishinda zawadi lakini cha muhimu alinishindia heshima katika kijiji chetu'', alisema akiongezea kuwa Ramu ana upendo mwingi licha ya kimo chake na hasira katika mashindano ya Jalikattu.
Kwa miaka mingi, watu wengi wamejeruhiwa ama hata kuuawa katika mashindano hayo.
Mamia wakiwemo mashabiki wameuawa ama hata kujeruhiwa .
Alimnunua wakati alipokuwa umri wa miaka 10.
Mmiliki wake alitaka kulipwa fedha nyingi lakini baadaye akakubali kumuuzia Ramu kwa kiwango cha chini baada ya kumwambia kwamba alitaka kumfuga ng'ombe huyo lakini hana kiwango cha fedha anachotaka.

Uamuzi wa bi Kanagarasu wa kumwangalia ng'ombe huyo badala ya kuolewa sio wa kawaida hususan katika maeneo ya mamshambani nchini India.
Anasema nduguze na watu wa familia yake walishangazwa na hatua hiyo lakini baadaye wakaikubali.
Na ukakamavu wake umemfanya aheshimiwe na familia yake na wanakijiji wengine, huku akiendelea kumfuga ng'ombe huyo anayempatia kipato cha kutosha .
Nyumba yake ndogo ina jiko na chumba kimoja cha kulalia, ambacho pia ndio sebule na eneo, la kulalia.
Yeye hupata kipato cha Rupee 200 ambazo ni sawa na dola 3.15 kwa siku na anatumia fedha zote kuhakikisha kuwa Ramu yuko katika hali nzuri.
Mbali na nyasi na matawi ya mchele wanayopewa ng'ombe wengi katika jimbo la Tamil Nadu , pia anakula nazi, tende, ndizi njugu, mtama na mchele.
Bi Kanagarasu alitaka kuendeleza
 utamaduni wa familia ya kufuga ngombe

'Kulikuwa na siku ambapo nilikula mara moja kwa siku ili niweze kuweka fedha za kumnunulia Ramu chakula'', anasema.
Mbali na chakula chake maalum, Ramu uhitaji mazoezi ya kila mara.
Hivyobasi bi Kanagarasu humchukua kila siku katika kidimbwi cha maji kilichopo kijijini ili aweze kuogelea kwa lengo la kuimarisha magoti yake.
''Binamu yangu Rajkumur pia humtembeza na kumfunza kukabiliana na wapinzani wake katika mchezo wa Jalikattu''.
''Pia hupata ripoti ya hali ya afya ya Ramu kutoka kwa daktari wa wanyama kabla ya kila shindano la Jalikattu ili kuhakikisha kuwa Ramu anafuzu'', anasema
Bi Kanagarasu humpatia ramu
chakula maalum na pia kuangalia afya yake.
Kutokana na ufanisi wa Ramu katika mashindano ya Jalikattu, watu wengi wametaka kumnunua ng'ombe huyo.
Mmoja wa ndugu zake Indira Selvaraj anasema alikataa ombi la hadi Rupee 100,000 kumuuza Ramu.
Anataka kumfuga ng'ombe huyo,kumuandaa kwa mashindano ya Jalikattu ndio lengo kuu la maisha yake.
Tulishindwa kumshawishi kukubali ombi letu. Sasa tumekubali kwamba hakuna gharama ya kufuta malengo ya mtu..
Zaidi 

Jeshi la polisi lakanusha kukamata wanaovaa

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuwepo kwa operesheni ya kuwakamata watu wanaovaa nguo fupi maarufu kama ‘vimini’ na milegezo katika mkoa huo.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,
Lazaro Mambosasa

Limesema operesheni yake ni ya kukamata watu wanaovaa nguo fupi na kina dada wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kuwa hao wanatenda kosa kinyume cha sheria ya nchi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alikuwa akifafanua taarifa iliyoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kuna operesheni ya kukamata wanaovaa nguo fupi.
Alisema hayo alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari na kulikuwa na swali kuhusu ukamataji wa watu wanaovaa nguo fupi ambapo alisema hakuna msako wa namna hiyo badala yake, alisema, Polisi wanakamata watu wanaofanya vitendo vinavyovunja sheria iliyotungwa na mamlaka zilizopewa dhamana na siyo kuwakamata wanaovaa nguo fupi.
Alisema alichokieleza  ni kuwa inategemea ni wapi ulipovalia nguo hizo na kueleza kwa mfano eneo la fukweni ’beach’ ambalo ni eneo watu kustarehe hawategemei mtu aende na makoti mazito na suti katika maeneo hayo kwa kuwa kuna nguo zake rasmi za kuogelea huko.
Alisema nguo fupi inategemea inavaliwa wapi na watashangaa mtu atakayevaa nguo fupi akakutwa kanisani au mahali penye staha. “Sikueleza kama kuna msako watu wanaovaa nguo fupi isipokuwa nilichokisema ni kwamba kuna matendo mtu anaweza kuyafanya ambayo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania. Watanzania wana utamaduni wao wa mavazi, mavazi mafupi ni kuiga tamaduni za wageni ambapo kwao hata wakija huku wanakuwa na nguo zinazokubalika mataifa yao,”alisema.

Alhamisi, 18 Januari 2018

Tanzania yafuta usajili wa meli mbili zilizokua na Madawa ya kulevya

Serikali ya Tanzania imetangaza kuunda kamati ya pamoja ya wataalam bara na visiwani itakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kupitiwa upya usajili uliokwishafanyika na kuzihakiki taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini, kuangalia mwenendo mzima wa usajili, na hatimaye kutoa mapendekezo na ushauri kwa Serikali.
Moja ya meli zilizosajiliwa Tanzania 🇹🇿 

Hatua hiyo inachukuliwa baada ya taarifa ya kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na umma juu ya hatua zinazochukuliwa na kukamatwa kwa meli hizo za Kaluba yenye usajili namba IMO 6828753 iliyokamatwa mwishoni mwa mwaka jana na wastani wa kilo 1,600 za dawa za kulevya katika maeneo ya Jamhuri ya Dominican Republic; na
Andromeda yenye namba za usajili IMO 7614666 iliyokamatwa ikisafirisha silaha kinyume na Sheria za kimataifa.
Makamu wa Rais amefahamisha kuwa Tanzania ilitoa kibali kwa kwa Jeshi la Mwambao wa Marekani na Jeshi la Mwambao wa Ugiriki kuweza kuzikamata na kuzipekua meli hizo.
Na baada ya upekuzi, hatua za haraka zilizochukuliwa na Tanzania ni kufuta Usajili wa Meli hizo.
Makamu wa Rais amesema piua taarifa za kukamatwa kwa meli hizo zimeleta mshtuko mkubwa ndani ya nchi, kutokana na kwamba Tanzania imejipambanua kupambana na maovu hayo kwa nguvu zake zote.
Meli hizo mbili zilisajiliwa Tanzania kupitia taasisi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar ambayo ndiyo imepewa mamlaka ya kusajili meli za nje.
Usajili wa Meli za Nje hufanywa na nchi nyingi duniani, ambapo Afrika nchi zinazofanya usajili wa kimataifa ni pamoja na Liberia, Komoro na Sierra Leone. Aidha, kwa Bara la Asia, ni pamoja na China na Singapore. Na Amerika ya Kusini ni pamoja na Panama.
Aidha imebainika kuwa wenye Meli hupendelea kusajili meli zao nje ya nchi zao kwa kukimbia uzito wa kodi na sheria zinazobana shughuli zao.
By Dickison Baraka 

John Pombe Magufuli kupiga marufuku michango yote katika shule nchini

Kufuatia msimamo wa Raisi John Pombe Magufuli kupiga marufuku michango yote katika shule nchini wadau wa sekta ya elimu wamekuwa na maoni mbali mbali


Michango hii imekuwa ikisaidia shughuli mbali mbali za maendeleo katika shule ikiwemo kusaidia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi sambamba na mahitaji mengine muhimu kwa shule hizo ikiwemo maji na ulinzi
Meneja wa miradi ya haki elimu nchini Tanzania bwana Bonventure Geofrey amesema tamko hilo linashitusha kufuatia hali halisi ya shule nchini Tanzanaia kuwa zenye changamoto kubwa ikiwemo uchakavu na uhaba wa miundombinu kama vile madarasa , vyoo na maabara kwa shule za sekondari
Akizungumza baada ya tamko hilo waziri wa elimu sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi Joyce Ndalichako amewataka waalimu wote ambao tayari walikuwa wamekwisha kuchangisha fedha hizo kufanya utaratibu wa kurejesha kwa wazazi michango hiyo na kutoendelea tena na utaratibu huo ulipigwa marufuku. 
Serikali ya wamu ya tano nchini Tanzania ilitangaza kutoa elimu bure katika ngazi ya elimu msingi ambayo ni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Rais wa Tanzania amesema kwamba walimu watakaopatikana wakiwalipisha fedha wazazi ili kulipia elimu ya wanao watafutwa kazi.
Serikali ilianzisha elimu ya bila malipo katika shule za majimbo yote nchini humo mwaka 2015 .
Lakini rais Magufuli amesema kuwa baadhi ya shule zinaendelea kulipisha karo na malipo mengine ya chakula, ziara za masomo na huduma nyenginezo.
Wanafunzi wasiolipa fedha hizo hulazimika kurudi nyumbani .

Jumatano, 17 Januari 2018

UGONJWA WA INI NI HATARI ZAIDI KULIKO UKIMWI, FAHAMU DALILI NA KINGA YAKE


HEPATITIS B
Ugonjwa wa Homa ya ini(Hepatitis B) unaaminika kuwa hatari zaidi kuliko hata UKIMWI.

HOMA YA INI (HEPATITIS B)









Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu. Virusi hivyo vinaitwa HBV(Hepatitis B Virus).

Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Inakadiriwa takribani watu 600,000 wanapoteza maisha Duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini kila mwaka.

Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye kifo.
MAAMBUKIZI.

Kama ilivyo kwa UKIMWI, virusi vya homa ya Ini huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu. Lakini pia HBV husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwamtoto wakati wa kuzaliwa.

NA HIZI NDIO NJIA KUU ZA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI (HEPATITIS B)

1.Kujamiana bila kinga
2.Kunyonyana ndimi
3.Mama kwenda kwa motto wakati wa kujifungua
4.Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano n.k
5.Kuchangia miswaki
6.Kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo
7.Kuchangia damu isiyo salama
8.Kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho

TAFITI ZA KITAALAMU ZINAONYESHA KUWA VIRUSI HIVYO NI HATARI KULIKO HATA VYA UKIMWI,
 UNAJUA KWANINI?

Virusi hivi vina uwezo wa kuishi nje ya mwili wa binadamu(yaani nje ya mfumo wa damu mpaka siku saba).

Virusi vya UKIMWI(VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.

Tafsiri yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180.

Ndani ya siku 30 mpaka siku 60, mtu mwenye HBVanaweza kugundulika ikiwa atapimwa. 
Mtu mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye UKIMWI.

DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA INI (HEPATITIS B)

Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.

Hata hivyo watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. 

Dalili hizo ni,
1.Uchovu
2.Kichefuchefu
3.Mwili kuwa dhaifu
4.Homa kali
5.Kupoteza hamu ya kula
6.Kupungua usito
7.Maumivu makali ya tumbo upande wa kulia
8.Macho na ngozi kuwa vya njano
9.Mkojo mweusiKwa wagonjwa wengine, 
Pia fahamu virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika kabisa. Hali hii huitwa saratani ya Ini.

                         TIBA
Mpaka sasa homa ya Ini haina tiba, lakini habari njema ni kwamba kuna chanjo.

NB : Ugonjwa huu ukishafika hatua ya ini kuharibika (Saratani ya ini) maana yake kinachofuata ni kifo.

Pamoja na kutokuwepo tiba, kuna chanjo ambayo iwapo ukiipata itakuepusha na maambukizi.

Chanjo za ugonjwa huu hutolewa hospitali kote nchini na hutolewa mara tatu.

Kwa ambae hajaambukizwa chanjo humuepusha kabisa na ugonjwa huu. Hivyo ni muhimu sana.

Kwa aliyeambukizwa chanjo humsaidia kuisha zaidi ya miaka 20, hivyo ni muhimu sana kupata chanjo.

Asilimia 30-50 ya watoto chini ya miaka 6, Hepatitis B hukua mpaka kuwa sugu na baadaye nikifo.

Asilimia 90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyohutoweka ndani ya miezi sita. Yaani uimara wa ini husababisha virusi kupotea.

JE WAJUA ACHA NIKUJUZE LEO!

1. Linajulikana kama Burj Khalifa ndio Jengo refu kuliko yote duniani lililopo Dubai ambalo limeenda angani mita 828 toka ardhini.
Burj Khalifa-Dubai

Lina ghorofa zipatazo 160 ambazo ni nyingi sana kulinganisha na jengo lililokuwa likijulikana awali kama ndilo refu kuliko yote duniani la Taipei lenye ghorofa 101.Ghorofa hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2004, mbali ya kuwa jengo refu kuliko yote duniani ndilo pia jengo lenye lifti ndefu kuliko zote duniani.

2. Fahamu pikipiki aina ya Dodge Tomahawk,350 mph 
Ndio yenye kasi zaidi kuliko zote ulimwenguni ina uwezo wa kwenda 560km/h pia ina uwezo wa kuzalisha horsepower 500 (370kw),Pikipiki hii ina cylinder 10, 90 degree v-type engine.
Dodge Tomahawk

Inaweza kufika spidi ya 350 mph (560 km/h).Inaweza kuzalisha 500 horsepower (370kw), huku ikifwatiwa na Suzuki Hayabusa, MTT Turbine Superbike Y2K
Tazama video hapa👇
  

Jumanne, 9 Januari 2018

Watu 30 wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali za kaunti ya Mombasa pwani mwa Kenya baada ya kuugua ugonjwa wa Chikungunya

Watu 30 wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali za kaunti ya Mombasa pwani mwa Kenya baada ya kuugua ugonjwa wa Chikungunya, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali KBC.
Gavana wa Mombasa Hassan Joho, amezindua magari matano yenye mashine na dawa kunyunyisiwa katika kaunti hiyo wakati ugonjwa unazidi kuwatishia watu zaidi.
Chini ya miezi mitatu iliyopita kaunti ya Mombasa ilikuwa ikikabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo watu kadha walilazwa hospitalini na maeneo kadhaa ya mankuli kufungwa katika kaunti hiyo.
Joho alithibitisha kuwa kumekuwa na visa 120 vya wagonjwa na imethibitwa kuwa visa 32 kati ya hivyo ni vya ugonjwa wa chikungunya.
Kufuatia ugonjwa huo kusambazwa na mbu Gavana Joho amewashauri wenjeji wa mombasa kushirikiana kwa karibu na serikali ya kaunti kuondoa mazingira salama kwa mbu.
Watu 32 hawajulikani waliko baada ya meli ya mafuta na ile ya mizigo kugongana mashariki mwa pwani ya China Jumamosi jioni.
Meli ya mafuta ya Sanchi yenye usajili wa Panama ikibeba tani 136,000 za mafuta kutoka Iran ilishika moto baada ya kugongana.
Wizara ya uchukuzi nchini China ilisema kuwa watu ambao hawakulinai wali ni wahudumu wa meli wakiwemo 30 raia wa Iran na wawili kutoka Bangladesh.
Wahudumu 21 wa meli ya mizigo wameokolewa.
Picha iliyochapishwa na kituo cha taifa cha CGTN, ilionyesha moto mkubwa na moshi ukitoka kwenye meli ya mafuta.
Ajali hiyo ilitokea karibu kilomita 296 kutoka pwani ya Shanghai.
Meli nane za China zimetimiwa kwa oparesheni ya uokoaji kwa mujibu wa shirika la Xinhua nchini China.
Korea Kusini nayo imetuma meli ya walinzi wa pwani na helikopta kusaidia katika uokoaji.
Meli ya mizigo ya usaljili wa Hog Kong CF Crystal ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka kutoka Marekani kwenda mkoa wa Guangdong kusini mwa China.

TAMBUA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufan...