Jumanne, 20 Februari 2018

Wasichana wa shule wanusulika kutekwa na Boko Haram


Wasichana wa shule na walimu kaskazini mashariki mwa Nigeria wamefanikiwa kukimbia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kwenye shule yao.
Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.
Kusikia sauti hizo wanafunzi na walimu wao walifanikiwa kutoroka.
Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.
Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana.
Baada ya kupata shule ikiwa bila mtu wanamgambo hao waliipora.



Image capti

Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo.
Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.
Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa.
Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko.
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

TAMBUA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufan...