Ijumaa, 20 Aprili 2018

SIRI YA KUFANIKIWA KIMAISHA




Wanadamu wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi vyema katika ulimwengu huu. kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao wamebahatika.

Hakuna watu waliozaliwa na bahati au mikosi, wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. yapo mambo kadha wa kadha ambayo inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha mazuri.

Umakini na nidhamu. 








Nidhamu inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. hakikisha unakuwa na ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila siku. hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.

Dhamira. 



Uaminifu umekuwa adimu sana kwa watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa kufanya ubadhilifu. ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.watu waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako na kufanya heshima yako ipotee. kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima kuliko kuijenga.

Usiwe na matumizi yasiyo na msingi. 



Watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. hakuna haja ya kutafuta sifa mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya. weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo ulipo.

Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. 



Uvivu wa kufikiri na wa kufanya kazi unakwamisha maendeleo. tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. tuache ubishoo wakuona kuwa kuna kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.
Kuwa mbunifu, lakini pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako. mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza Mungu utafanikiwa tu

Jumatatu, 2 Aprili 2018

FAHAMU FAIDA ZA JANI LA KIASILI MCHAICHAI KATIKA MWILI WAKO

MCHAICHAI


Ni wengi wanaoutumia na
kuufahamu mchaichai kama
kiungo cha chakula jikoni na
wengine hutumia kama dawa ya
mbu.
Lakini, je unafahamu kuwa
majani haya yana faida kubwa
kiafya . Mafuta ya mchachai
hutumika katika viwanda
vinavyotengeneza pafyumu na
sabuni.

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa
mchaichai una vichocheo
muhimu vinavyoweza
kupambana na athari kadha wa
kadha tumboni, kwenye mkojo
na hata kwenye vidonda. Watu
wengine huamini kuwa
mchaichai unaweza kutibu
baadhi ya maradhi kama vile
homa ya matumbo, matatizo ya
ngozi, madhara yanayotokana
na ulaji wa chakula chenye
uchafu na pia hutibu maradhi
ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa
kinywaji kinachoweza
kupunguza joto. Chai ya
mchaichai inasaidia kupunguza
joto kwa mgonjwa wa homa.

Faida nyingine za mchaichai
kiafya ni pamoja na:

1.KINGA DHIDI YA SARATANI

Tafiti mbalimbali zimeonyesha
kuwa kwenye kila gram 100 ya
mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya
ugonjwa wa saratani. Mwaka
2006, timu ya watafiti kutoka
Chuo kikuu cha Gurion, Israel
waligundua mchaichai una
uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.

2.MMENG'ENYO WA CHAKULA

-Husaidia umeng’enyaji wa
chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha
utaratibu wa mmeng’enyo wa
chakula na pia hutibu
magonjwa ya kuhara na
maumivu ya tumbo ikiwamo
kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa
kuondoa uchafu mwilini
Katika matibabu,
unatibu magonjwa
mengi ikiwemo
kushusha joto, hasa kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na
malaria kali.

3. KUSAFISHA FIGO NA MKOJO

Mchaichai pia una kazi ya
kusafisha figo ambayo kazi yake
kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta
mabaya mwilini ambayo mengi
yanatengenezwa na kemikali
kiwandani na hivyo mwili
kushindwa kuziondoa na
baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo
saratani.

Figo inapokuwa safi na imara,
hata kazi nyingine kama
kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi kwani mkojo unapozidi
kuwa mchafu mtu hujikuta
akivimba mwili na wakati
mwingine kufikia hata hatua ya
kupoteza maisha.

4.MAUMIVU WAKATI WA HEDHI

Mchaichai pia huwasaidia kina
mama ambao wanaumwa na
tumbo kipindi cha hedhi, ambao
wengi wao huchukulia kama
chango.
“Unapokunywa mchaichai,
unawezesha kusafisha mirija ya
uzazi na hivyo kuwezesha damu
kupita kwa urahisi,”

5.MAJIPU NA MCHAFUKO WA DAMU

vilevile mchaichai una
kazi ya kusafisha damu, hasa
kwa watu ambao wamekuwa na
tabia ya kupata magonjwa ya
ngozi kama mapele na kutoka
majipu

6.KUZUIA KUHARISHA

Mchaichai pia unaelezwa kuwa
ni dawa ya kuzuia kuharisha
ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya
protozoa anayesababisha
ugonjwa huo.

7.MAMA WAJAWAZITO

Endapo mjamzito atatumia
majani ya mmea huu kwa muda
mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji
kwani husaidia katika kulegeza
nyonga ambazo hubana katika
kipindi cha ujauzito na kufanya
njia kuwa ndogo kuwezesha
mtoto kupita,

8.VIDONDA VYA TUMBO

Hata hivyo kwa wagonjwa
wanaosumbuliwa hasa na
vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia
kuondoa gesi ambazo huwapata
mara kwa mara.

9.HUONGEZA CD4

Kwa wagonjwa wa ukimwi,
mchaichai unaelezwa kuwa
huongeza CD4 na inashauriwa
kuwa ni vyema mgonjwa wa
aina hiyo akapendelea kutumia
zaidi mchaichai kuliko majani
ya chai.

Kama hutumii basi una shauri kuanza kutumia mchaichai

TAMBUA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufan...