Jumanne, 20 Februari 2018

Wasichana wa shule wanusulika kutekwa na Boko Haram


Wasichana wa shule na walimu kaskazini mashariki mwa Nigeria wamefanikiwa kukimbia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kwenye shule yao.
Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.
Kusikia sauti hizo wanafunzi na walimu wao walifanikiwa kutoroka.
Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.
Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana.
Baada ya kupata shule ikiwa bila mtu wanamgambo hao waliipora.



Image capti

Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo.
Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.
Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa.
Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko.
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mchekeshaji wa miaka 7 kutoka Nigeria afika Hollywood

Mchekeshaji maarufu kutoka Nigeria, Emmanuella Samuel, ametangaza anaenda kufanya kazi na kampuni kubwa ya filamu za watoto, Disney nchini Marekani.
Emanuella Ella Angel ni mchekeshaji mwenye umri wa miaka saba ametangaza taarifa hizo katika ukurasa wake wa Instagram alipoweka picha yake akiwa katika harakati za kurekodi.
Katika ujumbe wake aliwashukuru mashabiki wake wote na kusema: "Sikuwahi ota nitafika hapa mapema hivi"
Emmanuella ni mhusika wa kurasa wa Youtube yenye mafanikio makubwa ya Mark Angel Comedy.
Ukurasa huo hupata mamilioni ya watazamaji. Kama video hii iliyopata zaidia ya watazamaji milioni saba.

Amepata pongezi kutoka watu wengi Nigeria wenye vyeo vikubwa akiwemo rais wa bunge la senate wa Nigeria.

 Hii ni moja wapo ya video

Jumamosi, 10 Februari 2018

Alexis Sanchez ahukumiwa kifungo cha miezi 16 jela la sivyo alipe faini

Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.
Hukumu hiyo imetolewa jana ,Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake kulipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.
Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.
Alexis Sanchez

TAMBUA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufan...