Ijumaa, 15 Desemba 2017

Baa 24 za fungiwa Unguja

Mahakama  ya Vileo Zanzibar imezifungia jumla ya baa 45 zilizopo Unguja kutoendelea kufanya biashara ya pombe kwa mwaka 2018 kutokana na kukosa vigezo vya kimazingira na kisheria.
Akitoa Uwamuzi huo Mwenyekiti wa Mahakama hiyo Mohammed Subeit amesema bodi ya vileo ilifanya ziara kila Mkoa na Wilaya kufanya utafiti wa baa na kugundua baa hizo hazina sifa wala vigenzo vya kufanya biashara hiyo.


Amesema katika ukaguzi wake walipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya baa hasa zile zilizopo katika makaazi ya jamii na kuamua kufanya tafiti na ilipojiridhisha iliamua kuyaondoa maombi ya wamiliki wa baa.
Hata hivyo amewataka wamiliki wa baa ambao hawakuridhika na maamuzi ya mahakama yaVileo nafasi ipo wazi ya kupindua maamuzi yale na  kukata rufaa mahakama kuu kama wanahisi hawakutendewa haki.
Kwaupande wao baadhi ya wamiliki wa baa wamesema hawakuridhia maamuzi yaliyotolewa na Mahakama na kuahidi kukata rufaa mahakama kuu ili kuendelea na biashara hiyo kwa mwaka 2018.
Nao baadhi ya wananchi wamesema wamefurahisha na maamuzi ya mahakama ya kuzifungia baa hizo lakini  nao wataka rufaa ili kuzipinga baa zilizopewa vibali vya pombe kuendelea na biashara hiyo kwani bado zinaleta usumbufu katika makaazi ya jamii ikiwemo vitendo vya udhalilishaji,kuuza miili yao na ukahaba.
Baa zilizofungiwa katika Mkoa wa kusini Unguja 14,Mkoa wa kaskazini Unguja 15 na kwa Mkoa wa Mjini Magharibi 16 kutoendelea kufanya biashara kwa mwaka 2018.

Dickison Baraka

TAMBUA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufan...